99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Tanzania kuimarisha uchunguzi na matibabu ya saratani kwa teknolojia ya nyuklia

(CRI Online) Novemba 13, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amesema mipango inaendelea ya kuimarisha vituo vya uchunguzi na matibabu ya saratani kwa teknolojia ya nyuklia Tanzania Bara na Zanzibar.

Rais Samia amesema mpango wa kuimarisha vituo vya matibabu kwa nyuklia kudhibiti saratani, mbinu ambayo hutumia mionzi kusaidia kutambua na kutibu ugonjwa huo, utagharimu euro milioni 59.

Taarifa hiyo imetolewa kwa niaba yake na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi kwenye uzinduzi wa maabara na ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania katika visiwa vya Zanzibar.

Rais Mwinyi amesema vituo vya uchunguzi na matibabu ya saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam, Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza na Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma vitaimarishwa.

Wizara ya Afya ya Tanzania imesema watu elfu 44 hugunduliwa kila mwaka kuwa na saratani nchini humo, na mwaka 2020 watu zaidi ya elfu 26 walifariki kutokana na ugonjwa huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha