99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ushirikiano kati ya China na Afrika waimarisha ujenzi wa jamii yenye ustahimilivu

(CRI Online) Novemba 12, 2024

Maofisa wa Umoja wa Afrika (AU) na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), wamesema ushirikiano kati ya China na Afrika unaendelea kushika kasi kuelekea kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye ustahimilivu na mustakabali wa pamoja.

Maofisa hao wamesema hayo kwenye semina iliyofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya kaulimbiu ya "kujenga pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya".

Semina hiyo ni ni mwendelezo wa mkutano wa FOCAC uliofanyika Septemba mjini Beijing, na kufafanua njia halisi za kujenga jumuiya hiyo yenye lengo la pamoja na kuheshimiana.

Mkurugenzi wa uhusiano wa nje na ushirikiano wa kimkakati wa Africa CDC Bibi Claudia Shilumani, amesema China na Afrika zinajenga mfumo wa afya wa kisasa unaoweza kuhimili na kukabiliana na changamoto za sasa za afya barani Afrika, na kuendeleza wafanyakazi wa afya wenye ujuzi ili kuhakikisha waafrika wananufaika na maendeleo ya usalama wa afya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha