

Lugha Nyingine
Jinsi CIIE inavyokuwa kichocheo cha Ushirikiano na Ustawi wa Pamoja kati ya China na Afrika
Picha iliyopigwa Novemba 4, 2024 ikionesha Kituo cha kitaifa cha Mikutano na Maonesho cha Shanghai , ambapo ni kituo kikuu cha Maonesho ya saba ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE). (Xinhua/Yin Gang)
Maonesho ya saba ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yamefunguliwa Shanghai, China wiki hii, ambapo zimeoneshwa Bidhaa mbalimbali kutoka nchi za Afrika, huku mazungumzo ya uwekezaji yakifanyika kwa kulenga kubadilisha soko kubwa la China kuwa fursa kubwa.
Watu wakitembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya saba ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai, Novemba 5, 2024. (Zhou Xinyi/Xinhua)
Tangu maonesho hayo ya kwanza yalipofanyika mwaka 2018, maonesho hayo yametumia vya kutosha nguvu bora ya soko kubwa la China na yamekuwa jukwaa muhimu la manunuzi ya kimataifa, uhimizaji wa uwekezaji, na ufunguaji mlango na ushirikiano. Kadiri China ilivyofungua mlango zaidi kwa Afrika, ndivyo mazao mengi ya kilimo yanavyooneshwa zaidi kwenye maonesho ya CIIE ili kupata nafasi kwenye soko la China.
Kahawa ya Ethiopia ni bidhaa inayooneshwa kila mara kwenye maonesho hayo. Tangu ilipooneshwa kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo mwaka 2019, kahawa ya Ethiopia imetambuliwa na kujulikana kwa watu wengi zaidi kwenye soko la China, alisema Ruth Wondosen Tesfaye kutoka Addis Coffee.
“Maonesho ya CIIE imetoa jukwaa la kipekee la kuwasiliana moja kwa moja na wateja na wauzaji, ni jukwaa lenye thamani sana kwa kuimarisha mikakati yetu ya uuzaji bidhaa zetu kwa nje,” Ruth aliliambia shirika la habari la China Xinhua huko Shanghai.
Asali ya Tanzania pia imeonekana kwa mara ya kwanza kwenye maonesho hayo mwaka huu. “Maonesho hayo ni fursa muhimu kwa kampuni za asali za Tanzania, kwa kuwa siyo tu yametandika njia kwa bidhaa zetu kuingia kwenye soko la China, bali pia ni hatua muhimu kwa chapa za asali ya Tanzania kuingia kwenye soko la dunia ” alisema Jackson Mponela, meneja wa uzalishaji wa kampuni ya Tanzania Enterprises.
Kampuni ya Khozeni Farming kutoka Afrika Kusini imeshiriki kwa mara ya kwanza na maparachichi yake kwenye maonesho ya mwaka huu. Nkateko Khoza, ofisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo, aliliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa soko la China litaleta fursa mpya ya ongezeko kwa viwanda vya parachichi vya Afrika Kusini.
Watu wakipiga picha kwenye banda la Afrika Kusini kwenye Maonesho ya saba ya kimataifa ya uagizaji bidhaa ya China (CIIE) huko Shanghai, China Novemba 6, 2023. (Xinhua/Fang Zhe)
Tangu Mkutano wa Mawaziri wa FOCAC 2021 ulipofanyika, China na Afrika zimehimiza kwa hatua madhubuti utekelezaji wa mapendekezo ya jukwaa hilo, likiwemo kuweka “njia ya kijani” kwa mazao ya kilimo ya Afrika kuingia kwenye soko la China.
Mwaka huu kwenye maonesho ya CIIE, bidhaa za maeneo ya Kusini ya Dunia imefuatiliwa zaidi. Mkutano wa 7 wa Jukwaa la Uchumi wa kimataifa la Hongqiao umechukua mada ya “Maendeleo Endelevu kwa Nchi za Kusini na Ushirikiano kati ya China na Afrika” kuwa mada muhimu ya majadiliano, ukilenga kutoa maoni na mapendekezo kwa ajili ya nchi zilizoko nyuma kimaendeleo kuhimiza ongezeko la kunufaisha wote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma