99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kituo cha Ufanisi cha China, Afrika na UNIDO chafunguliwa nchini Ethiopia

(CRI Online) Novemba 06, 2024

China, Ethiopia na Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa (UNIDO) zimezindua kituo cha ufanisi mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, ili kuboresha mageuzi endelevu ya viwanda, kilimo cha kisasa na maendeleo ya ujuzi barani Afrika.

Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho kilicho ndani ya Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi Stadi mjini Addis Ababa, ilifanyika jumatatu wiki hii, na maofisa wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China na maofisa wa ngazi ya juu wa UNIDO wameshiriki kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa UNICO Gerd Muller amesema, kituo hicho kitaleta teknolojia mpya katika teknolojia ya kilimo, nishati mpya na mambo ya kidijitali nchini Ethiopia na bara zima la Afrika.

Ubalozi wa China nchini Ethiopia umesema, kwa juhudi za pamoja za pande husika, kituo hicho cha ufanisi kitaweka mkazo katika kuwaandaa vipaji zaidi na kuhamisha teknolojia kwa Ethiopia na nchi nyingine za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha