99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Wafanyabiashara Tanzania Zanzibar kutozwa kodi ndogo

(CRI Online) Oktoba 29, 2024

Rais wa Visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi ameziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka viwango vidogo vya tozo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri.

Rais Mwinyi amesema hayo alipokuwa akifungua soko jipya la kisasa la Jumbi katika Mkoa wa Mjini Magharibi, akiwahakikishia wafanyabiashara kuwa serikali itaendelea kuwaandalia mazingira bora zaidi yatakayoendana na soko hilo.

Rais Mwinyi amesisitiza kuwa serikali ya Zanzibar imetenga shillingi bilioni 100 kwa ajili ya kuwapatia mitaji wajasiriamali na wafanyabiashara kuimarisha biashara zao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha