99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Makamu wa Rais wa Tanzania atoa wito wa kuongeza thamani ya madini

(CRI Online) Oktoba 22, 2024

Makamu wa Rais wa Tanzania Bw. Philip Mpango ametoa wito wa kuongezwa kwa thamani ya madini ya nchi hiyo.

“Hatupaswi pekee kuchimba madini na kuuza nje yakiwa ghafi bali pia kuyaongezea thamani ndani ya nchi” Bw. Mpango amesema alipohudhuria maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) mjini Dar es Salaam.

Amezitaka taasisi za utafiti kuainisha maeneo ya ukuaji wa uchumi na mikakati ili kutumia kikamilifu fursa za sekta ya madini, ambazo zinaweza kutumika kuijenga Tanzania kuwa nchi ya kipato cha juu ifikapo mwaka 2050.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha