99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ushirikiano kati ya Angola na China wachochea maendeleo ya pamoja

(CRI Online) Oktoba 16, 2024

Katibu wa idara ya sera na uendelezaji wa makada ya chama tawala cha Angola MPLA, Angela Braganca amesema, ushirikiano wa muda mrefu kati ya Angola na China umeimarisha urafiki kati ya nchi hizo, na kuchochea maendeleo na ustawi wa pamoja.

Akizungumza katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa 6 wa Mwaka kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ya China, Bi. Braganca amesisitiza umuhimu wa mabadilishano ya kitamaduni na kielimu kati ya China na Angola, akisema moja ya ajenda muhimu ya mkutano huo inayohusu uzoefu wa China katika kuondokana na umasikini, ina umuhimu mkubwa kwa uongozi wa Angola.

Mkutano huo ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Renmin cha China, unatarajiwa kumalizika kesho Alhamisi kwa majadiliano kati ya wasomi na wawakilishi kutoka China na wajumbe wa MPLA na wasomi wa Angola kuhusu njia za kuondokana na umasikini, ushirikiano kati ya China na Afrika, na utandawazi wa kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha