99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uchumi wa Somalia kukua kwa asilimia 3.7 mwaka huu

(CRI Online) Oktoba 15, 2024

Uchumi wa Somalia unatarajiwa kuimarika hadi ukuaji wa asilimia 3.7 mwaka huu na asilimia 3.8 mwaka 2025.

Ripoti mpya ya Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB inasema ukuaji wa pato la taifa la Somalia utachochewa na kuimarika kwa sekta za mifugo, huduma, fedha zinazotumwa kutoka nje na uwekezaji.

Eneo la kimkakati la nchi hiyo katika bahari ya shamu na bahari ya Hindi linaiweka Somalia kuwa kitovu cha usafirishaji cha kikanda kwenye ghuba.

Asilimia zaidi ya 80 ya mapato ya nje ya Somalia yanatokana na bidhaa za kilimo ambazo hazijasindikwa hivyo kuifanya nchi hiyo kukabiliwa na hali tete ya soko la bidhaa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha