99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Marais wa China na Russia wapongezana kwa kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili

(CRI Online) Oktoba 06, 2024

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin tarehe 2 wametumiana salamu za kupongeza miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Kwenye salamu zake, Rais Xi amesema China na Russia ni majirani, na pia ni nchi kubwa duniani, na nchi muhimu zinazoibuka kiuchumi. Na katika miaka 75 iliyopita, nchi hizo mbili zimeendelea kuinua kiwango cha uhusiano wao, kufuatilia maslahi ya kimsingi ya nchi na wananchi. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na Russia kupanua ushirikiano wao halisi, kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu na ujenzi wa mambo ya kisasa, na kutoa mchango mpya kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu duniani, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu.

Kwa upande wa Rais Putin, amesema hivi sasa kiwango cha uhusiano kati ya Russia na China kiko juu zaidi katika historia, nchi hizo mbili zimefanya ushirikiano katika nyanja mbalimbali zikiwemo siasa, uchumi na biashara, na sayansi na teknolojia, kuungana mkono katika mambo ya kimataifa na kikanda, na zinajitahidi kwa pamoja kujenga dunia yenye ncha kadhaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha