99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yapinga vitendo vyovyote vya kudhuru raia

(CRI Online) Septemba 25, 2024

Wizara ya Afya nchini Lebanon ilisema siku ya Jumatatu, kwamba mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa siku hiyo na Israel dhidi ya Lebanon yamesababisha vifo vya watu 492 na wengine 1,645 kujeruhiwa.

Akizungumzia mashambulizi hayo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian jana Jumanne alipokutana na wanahabari amesema, China inapinga vitendo vya kukiuka mamlaka ya kitaifa na usalama wa Lebanon, na kulaani vitendo vyovyote vinavyodhuru raia.

Bw. Lin amesema China inazitaka pande husika kuchukua hatua na kupunguza mvutano, kuzuia hali ya wasiwasi ya kanda hiyo kuwa mbaya zaidi, na kulinda utulivu wa kikanda na usalama wa maisha ya watu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha