99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kuunganishwa reli ya Ethiopia-Djibouti na bandari nchini Djibouti kunakuza biashara ya kikanda

(CRI Online) Septemba 11, 2024

Ofisa mkuu mtendaji wa Reli ya Ethiopia-Djibouti Bw. Takele Uma, amesema kuunganishwa kwa reli hiyo na bandari za kimkakati nchini Djibouti kunabadilisha biashara ya kikanda na ukuaji wa uchumi.

Amesema kuunganisha reli ya kilomita 752 iliyojengwa na China na bandari za kimkakati za Djibouti, kunabadilisha biashara ya kikanda, kukuza ukuaji wa uchumi wa nchi mbili zilizounganishwa, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.

Amesisitiza hitaji muhimu la kupanua zaidi fursa za usafirishaji kwa kurahisisha viunganishi vya bandari na reli. Pia amesema reli hiyo iliyojengwa na China inaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili za Pembe ya Afrika, na hatimaye kufungua njia ya ustawi wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha