99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kampuni za China kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme kwa jua nchini Namibia

(CRI Online) Septemba 10, 2024

Shirika la umeme linalomilikiwa na serikali ya Namibia, NamPower, limesaini makubaliano na kundi la kampuni za China kuhusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua, chenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, cha Rosh Pinah.

Makubaliano ujenzi wa mradi huo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 78, yatafanikisha mradi huo unaounga mkono juhudi za Namibia za kuimarisha miundombinu yake ya nishati mbadala, na unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa usalama na malengo endelevu ya usambazaji wa umeme nchini Namibia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Nampower Bw. Kahenge Haulofu amesema kituo hicho na miradi mingine ya miundombinu inayoendelea kujengwa, ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Biashara wa NamPower kwa kipindi cha 2020-2025.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha