99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yatoa waraka kuhusu mageuzi ya nishati

(CRI Online) Agosti 30, 2024

Idara ya Kiaifa ya Nishati ya China leo Alhamisi imetoa waraka kuhusu maguezi ya nishati. Waraka huo umeonesha kuwa, maendeleo ya nishati safi nchini China yamepiga hatua mpya kwa kufuata njia ya mageuzi inayoendana na hali halisi ya nchi na mahitaji ya zama za sasa.

Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, uwezo wa jumla wa mashine za kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo na jua nchini China umeongezeka kwa mara kumi kuliko miaka kumi iliyopita, na uzalishaji wa nyongeza wa umeme kwa nishati safi umechukua zaidi ya nusu ya matumizi ya nyongeza ya umeme nchini kote, huku matumizi ya nishati safi yakifikia asilimia 26.4 ya matumizi ya jumla ya nishati nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha