99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Hafla?ya kuwaaga?wanafunzi?wa Kenya waliopata?udhamini?wa masomo?wa serikali?ya China yafanyika?Nairobi

(CRI Online) Agosti 23, 2024

Shughuli ya kuwaaga wanafunzi wa Kenya waliopata udhamini wa masomo kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya kuendelea na masomo ya juu katika vyuo vikuu nchini China, imefanyika kwenye ubalozi wa China nchini Kenya.

Shughuli ya kuwaaga wanafunzi 13 walionufaika na udhamini huo, iliambatana na hafla ya kuwapatia tuzo washindi wa Shindano la Insha la "China-Africa Cooperation in My Eyes".

Maofisa waandamizi wa Kenya, wanadiplomasia, wanafunzi, wazazi, na walimu walishiriki kwenye hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Kenya Bibi Beatrice Inyangala, alipongeza ushirikiano imara kati ya Kenya na China katika sekta ya elimu ya juu na kuwapa ujuzi vijana wa Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha