99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kenya yazindua mpango elekezi wa utekelezaji wa haki unaozingatia mazingira yasiyo na uchafuzi

(CRI Online) Agosti 22, 2024

Mahakama ya Kenya imezindua mkakati elekezi ili kutetea ujumuishaji wa uendelevu wa mazingira katika mfumo wa haki nchini Kenya.

Jaji mkuu wa Kenya Bibi Martha Koome amesema mahakama imejitolea kutetea uendelevu wa mazingira kwenye makahama nchini Kenya, kwa kupitia kufuata sheria, kulinda haki za kuhakikisha maendeleo endelevu, na kuhimiza udumishaji wa ikolojia.

Akiongea mjini Nairobi kwenye uzinduzi wa mfumo huo, Bibi Koome amesema kwa kupitia mfumo huo, mahakama ya Kenya inathibitisha kujumuisha uendelevu wa mazingira katika utendaji wa mahakama za Kenya. Jaji mkuu pia amebainisha kuwa mahakama ya Kenya inaweka vigezo vya juu na kuwa mfano wa kufuatwa na sekta nyingine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha