99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Sudan yakabiliwa na hali mbaya inayotokana na mvua kubwa, mafuriko na mapigano yanayoendelea nchini humo

(CRI Online) Agosti 14, 2024

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, mvua kubwa, mafuriko na mapigano makali yanayoendelea yamesababisha hali kuwa mbaya zaidi nchini Sudan.

Ofisi hiyo imesema, mvua kubwa na mafuriko vimeathiri watu 143,000 katika majimbo 12 kati ya 18 ya nchini Sudan. Pia OCHA imesema mafuriko yamesababisha watu 27,000 kukosa makazi tangu mwezi Juni, huku mji wa El Fasher ukiwa umeathirika zaidi.

Wakati huohuo, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limeripoti kuwa limegawa chakula kwa watu karibu 14,000 katika eneo la Sheikan, Jimbo la Kordofan Kaskazini, ambalo ni moja ya maeneo yaliyofanyiwa tathmini na Kamati ya Kutathmini Njaa (IPC), kuwa liko katika hatari ya kukabiliwa na ukosefu wa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha