

Lugha Nyingine
Rais Paul Kagame aliyechaguliwa tena kuwa rais wa Rwanda aapishwa
(CRI Online) Agosti 12, 2024
(Picha inatoka Xinhua)
Rais Paul Kagame ambaye alichaguliwa tena kuwa rais wa Rwanda, ameapishwa jana katika Uwanja wa Amani wa Kitaifa wa Kigali, mji mkuu wa nchi hiyo.
Katika hotuba yake, rais Kagame amesema atachukua awamu yake mpya kama mwanzo wa kazi ngumu zaidi, na lengo kuu ni kuwahakikisha wananchi wanaishi maisha salama, yenye afya na heshima.
Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Afrika ya Kati, Msumbiji, na Kenya, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa na kikanda, na maofisa waandamizi wa serikali walishiriki kwenye hafla hiyo.
Rais Kagame alishinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika Julai 15, kwa kupata kura zaidi ya milioni 8.8, sawa na asilimia 99.18, na kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma