99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Magari yenye magurudumu matatu ya kutumia nishati ya umeme yanayotengenezwa na China?yabadilisha hali?ya ghuba ya punda katikati mwa Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 12, 2024

Peter Gitonga, Mwangi Githae na Maina Karuoho wakisubiri wateja katika ghuba ya punda ya Ruring'u huko Nyeri, katikati mwa Kenya, Agosti 5, 2024. (Picha na Robert Manyara/Xinhua)

Peter Gitonga, Mwangi Githae na Maina Karuoho wakisubiri wateja katika ghuba ya punda ya Ruring'u huko Nyeri, katikati mwa Kenya, Agosti 5, 2024. (Picha na Robert Manyara/Xinhua)

Kilomita mbili nje ya mitaa ya Nyeri, mji wa kati wa Kenya,kando ya barabara kuu inayounganisha mji huo na Nairobi, mtu hawezi kukosa kuona miti mikubwa ya kijani ambayo chini ya kivuli chake hupumzika makumi ya punda. Huko Nyeri na sehemu za pembezoni mwake, punda wamekuwa wakitumika kusafirisha bidhaa mbalimbali.

Katika miaka ya hivi karibuni, magari yenye magurudumu matatu ya kutumia nishati ya umeme yanayotengenezwa na China yakijulikana sana kama tuk-tuks, zimepata nafasi kubwa hatua kwa hatua kwenye yadi hiyo, ambayo ina zaidi ya punda 50 na mikokoteni.

Kuingizwa kwa tuk-tuk kumewafanya wafanyabiashara kuondokana na changamoto mbalimbali zilizowakabili hapo awali katika wakati wa kutumia punda.

Mwangi Githae ni mmoja wa wafanyabiashara wakongwe katika ghuba hiyo ambao wote wametumia magari ya tuk-tuk badala ya mikokoteni yao ya punda.

"Tumekuwa tukiacha kutumia punda badala yake kutumia tuk-tuk kutokana na magari yenye magurudumu matatu yanategemeka zaidi kuliko punda wa kubeba mizigo," Githae aliambia shirika la habari la China Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Uagizaji wa tuk-tuk kutoka China ulianzia miongo miwili hivi iliyopita, na kuleta urahisi kwa wafanyabiashara ambao hawakuwa na uwezo wa kununua magari, na baada ya hapo, matumizi ya tuk-tuk yameleta nafasi za ajira kwa watu na kuwa vyombo vya usafiri vya bei nafuu, vya usafiri wa haraka na wa kutegemeka zaidi kwa mamilioni ya Wakenya.

Mfalme wa Uingereza Charles III na Malkia Camilla wakifurahia usafiri wa Tuk Tuk walipotembelea huko Mombasa, Kenya, Novemba 3, 2023. (Picha na Fred Mutune/Xinhua)

Mfalme wa Uingereza Charles III na Malkia Camilla wakifurahia usafiri wa Tuk Tuk walipotembelea huko Mombasa, Kenya, Novemba 3, 2023. (Picha na Fred Mutune/Xinhua)

Bei ya Tuk-tuk moja nchini Kenya ni dola za Kimarekani kati ya 2,700 na 3,875, kwa kulingana na ujazo na chapa yake. Lakini, Gharama ya matumizi ya punda mmoja ilikuwa shilingi 7,000 tu (kama dola 54 za Kimarekani) na gharama ya utengenezaji wa mkokoteni ilikuwa dola 77.5 hivi. Akiwa na dola za Kimarekani 132 hivi tu, mtu mmoja peke yake aliweza kuanzisha shughuli bila matatizo.

Lakini kwa kulinganishwa na punda ambaye anaweza kusafiri umbali mfupi tu kila mara, gari lenye magurudumu matatu linaweza kusafiri kwa kilomita mia kadhaa kwa siku, na mwendo wake ni wa haraka, wenye ufanisi, na linaweza kubeba abiria na mizigo mizito zaidi.

Zaidi ya hayo, wafanyabiashara wamegundua tuk-tuk zikiwasaidia kuepusha matatizo mengi.

"Mara nyingi, tulikuwa na mizozo na wakulima baada ya punda kuingia kwenye mashamba yao na kuharibu mimea. Baadhi ya wakati, wakulima hao hata walishambulia na kuwajeruhi punda," Githae alisema, akiongeza kuwa kutafuta punda walipo kulipoteza muda wao mwingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha