99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Watu 17 wauawa katika mashambulizi ya vikosi vya RSF nchini Sudan

(CRI Online) Agosti 02, 2024

Watu takriban 17 wameuawa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa na Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) kwenye vijiji viwili vya jimbo la Gezira katikati mwa Sudan.

Kamati ya vita vya upinzani ya Wad Madani, mji mkuu wa Gezira imesema katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa wanamgambo wa RSF walivamia kijiji cha Al-Adnab wakiwa na misafara mikubwa ya kijeshi kwa lengo la kupora na kufanyia ukatili raia na kwamba watu zaidi ya 10 wameuawa kutokana na shambulizi hilo.

Aidha kamati hiyo imesema kuwa raia saba ambao hawakuwa na silaha pia wameuawa katika shambulizi la wanamgambo hao katika kijiji cha Wad Al-Asha siku ya Jumatano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha