99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais Xi Jinping ampongeza Kagame kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Rwanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 24, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumanne ametumia salamu za kumpongeza Paul Kagame kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Rwanda. Rais Xi ameeleza kuwa Rwanda ni nchi rafiki wa jadi wa China, na kwamba katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Rwanda umeendelea kwa kasi, huku matokeo yenye manufaa yakipatikana kwenye ushirikiano katika sekta mbalimbali na urafiki wa jadi ukiimarika kila siku.

Amesema angependa kushirikiana na Kagame katika kuongeza zaidi hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua na kuzidisha ushirikiano wenye manufaa halisi katika sekta mbalimbali, ili kuendeleza uhusiano wa pande mbili kwenye ngazi mpya.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha