

Lugha Nyingine
Pembe ya Afrika kuwa na joto kali kuliko kawaida katika kipindi cha miezi ya Agosti hadi Oktoba
Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa (ICPAC) cha Shirika la Kiserikali kwa Maendeleo la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) kimesema eneo la Pembe ya Afrika litakuwa na halijoto kali kuliko kawaida wakati wa msimu wa kipindi cha miezi ya Agosti mpaka Oktoba.
Kituo hicho kimesema, halijoto katika baadhi ya nchi za eneo hilo inaweza kupanda hadi nyuzi joto 35, na kwamba halijoto za kawaida hadi zile zenye baridi kuliko kawaida itashuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Sudan mashariki na maeneo ya karibu ya Ethiopia na Eritrea.
Licha ya viwango vya juu vya joto, ICPAC imesema, maeneo ya mashariki ya Pembe ya Afrika yanatarajiwa kuwa makavu kuliko kawaida wakati wa msimu wa kipindi cha miezi ya Agosti hadi Oktoba, huku maeneo ya kaskazini yakipata mvua kubwa kuliko kawaida.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma