99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Afrika Kusini yaadhimisha Siku ya Mandela

(CRI Online) Julai 19, 2024

Serikali ya Afrika Kusini na raia kutoka makundi na nyanja mbalimbali, wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela siku ya Alhamisi, ambayo pia inajulikana kama Siku ya Mandela, kwa kutoa michango yao chanya katika jamii kote nchini.

Katika taarifa yake serikali ya Afrika Kusini imesema Siku ya Mandela Mwaka 2024 ina umuhimu wa kipekee kwa sababu, katika siku kama hiyo mwaka 1994, Rais wa zamani wa nchi hiyo Mandela aliongoza Serikali ya kwanza ya Umoja wa Kitaifa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa mwaka 2024 ni maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa serikali ya kidemokrasia ya Afrika Kusini, hatua ambayo ni muhimu iliyofikiwa na Mandela, na duniani kote, ambapo amekuwa alama ya uhuru na demokrasia.

Msemaji wa serikali ya Afrika Kusini, Nomonde Mnukwa ametoa wito kwa watu binafsi, jamii na wafanyabiashara kuunga mkono mashirika ya hisani au kusaidia watu wasiojiweza, wakiwemo walioathirika na mafuriko na majanga mengine ya asili ambayo yameathiri nchi hiyo hivi karibuni, katika siku hii ya Mandela.

Siku ya Mandela, huadhimishwa kila mwaka Julai 18, tarehe ambayo ni siku ya kuzaliwa kwake na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Uwezo wa kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa bado uko mikononi mwetu".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha