99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

EAC na washirika wa IOM kuimarisha usalama wa afya katika mipaka ya kanda

(CRI Online) Julai 19, 2024

Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesema kwamba inashirikiana na Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) ili kuimarisha usalama wa afya wa kuvuka mipaka na kukabiliana na milipuko ya magonjwa katika maeneo ya mipakani.

EAC imetoa taarifa siku ya Alhamisi kwamba Kanda ya Afrika Mashariki yenye wakazi zaidi ya milioni 300, imeathiriwa na masuala ya usalama wa afya wa kuvuka mipaka na milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu, ebola, na janga la COVID-19 katika miaka michache iliyopita.

Taarifa hiyo imesema, katika baadhi ya nchi, milipuko hiyo imesababisha kuvunjika kabisa kwa mifumo ya afya ya umma, ambayo imeelemewa na kushindwa kuhimili hali.

Afisa mkuu wa afya wa EAC Eric Nzeyimana amesema kuwa EAC imeazimia kuwa na mawasiliano thabiti ya hatari na mkakati wa ushirikishwaji wa jamii ili kusimamia kwa ufanisi na kupunguza hatari zinazohusiana na dharura za afya ya umma na majanga mengine ya kiafya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha