99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Vyuo vikuu vya Kenya vyakumbatia karakana za Luban toka China ili kuwapa wanafunzi ujuzi

(CRI Online) Julai 11, 2024

Karakana ya Luban iliyoko Chuo Kikuu cha Machakos nchini Kenya inaendelea kutoa mafunzo katika vikundi vya watu sita, kuhusu namna ya kuunganisha sehemu mbalimbali za kompyuta.

Karakana hiyo ni moja ya idara muhimu katika Chuo Kikuu cha Machakos ambayo makumi ya wanafunzi wanapata mafunzo kila siku.

Chuo Kikuu cha Machakos kilianzisha karakana hiyo mwaka wa 2019 kwa msaada kutoka kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei na Chuo cha Ufundi cha Mji wa Tianjin (TCVC).

Wanafunzi katika karakana hiyo wamekuwa wakiipongeza karakana hiyo kwa kuchochea hisia na upendo kwa taaluma wanazosoma.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha