99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Madaktari wa China, UNESCO watoa huduma za matibabu bila malipo kwa kituo cha watoto yatima nchini Ghana

(CRI Online) Julai 09, 2024

Kundi la 13 la timu ya madaktari wa China nchini Ghana limeshirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutoa huduma za matibabu bila malipo kwa watoto yatima 61 katika Kituo cha Watoto yatima cha Motherly Love huko Kwabenya, mjini Accra, Ghana.

Watoto hao wenye umri wa miaka minne hadi 21, wamefanyiwa upimaji wa afya.

hang Rijia, mkuu wa kundi hilo la madaktari wa China amesema watoto hao wanahitaji msaada wa kimatibabu, na wanafurahia kupata fursa ya kuwatembelea na kutoa huduma za kimsingi za afya.

Mwakilishi wa UNESCO nchini Ghana Edmond Moukala amesema hatua hii inaonyesha kivitendo hatua inayochukuliwa kujenga kikamilifu jamii yenye amani na usawa.

Naye ofisa mtendaji mkuu wa kituo hicho cha watoto yatima Bw. John Azuma, ametoa shukrani kwa madaktari hao wa China na wale wa UNESCO.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha