99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa Jukwaa la Maendeleo ya Kijani la Nchi wanachama wa SCO

(CRI Online) Julai 08, 2024

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Jukwaa la Maendeleo ya Kijani la Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ambalo limefunguliwa leo Jumatatu kwenye mji wa Qingdao katika Mkoa Shandong, China.

Katika barua hiyo, Rais Xi amesema kulinda mazingira ya kiikolojia na kuhimiza maendeleo ya kijani, ni maoni ya pamoja ya nchi wanachama wa SCO.

Amesema, katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikishikilia kithabiti dhana ya kuzingatia usafi wa mazingira, na kufuata bila kuyumbayumba njia ya maendeleo mazuri inayojumuisha kuboreshwa kwa uzalishaji viwandani, maisha yenye ubora wa juu na mazingira mazuri ya ikolojia, ikisababisha mafanikio makubwa katika ujenzi wa China Nzuri.

Rais Xi pia amesema China inatumaini itaimarisha mawasiliano na ushirikiano katika nyanja ya maendeleo ya kijani na pande zote husika kupitia jukwaa hilo, ili kuwezesha maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii ya nchi zote wanachama na kuhimiza kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira asili.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha