99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

AfDB kufadhili mradi wa SGR unaounganisha Tanzania, Burundi na DRC

(CRI Online) Februari 26, 2024

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania zimetia saini makubaliano ya mkopo wa dola za kimarekani milioni 158.1 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa (SGR), kati ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).

Makubaliano hayo yamesainiwa kati ya meneja wa AfDB nchini Tanzania Bi. Patricia Laverley na Waziri wa Fedha wa Tanzania Bw. Mwigulu Nchemba mjini Dar es Salaam.

Bw. Nchemba amesema mradi huo una manufaa kwa Tanzania, kwakuwa utaimarisha uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi zisizo na bandari za DRC na Burundi. Bi. Laverley amesema kipaumbele kikuu cha AfDB ni kuziunganisha nchi za Afrika kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha