99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Sudan yakanusha madai ya Marekani kuhusu kuzuia ufikiaji wa msaada wa kibinadamu

(CRI Online) Februari 26, 2024

Sudan imekanusha na kupinga taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ya kuishutumu serikali ya Sudan kuzuia ufikiaji wa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa mgogoro wa Sudan.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema madai ya Marekani dhidi ya Jeshi la Sudan (SAF) na Serikali ya Sudan kuhusiana na misaada ya kibinadamu na shughuli za kiraia ni "shutuma za uongo”.

Taarifa ya Sudan imesisitiza ahadi ya serikali ya Sudan kwa Azimio la Jeddah kuhusu kulinda raia, lililosainiwa tarehe 11 mwezi Mei 2023.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha