99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Serikali ya Zanzibar yawahakikishia wadau wa utalii mazingira wezeshi

(CRI Online) Februari 21, 2024

Serikali ya Zanzibar imesisitiza dhamira yake ya kuboresha mazingira wezeshi ambapo kwa kushirikiana na wadau, serikali inatarajia kukuza zaidi utalii unaochangia asilimia 30 ya mapato ya serikali.

Waziri wa Utalii na Malikale wa Zanzibar Bw. Mudrik Ramadhan Soraga, amesema kuna nafasi ya kuboresha utendaji wa sekta hiyo.

Bw Soraga amesema hayo kwenye mkutano wenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wadau binafsi katika sekta ya utalii. Mkutano huo umeandaliwa na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar (ZCT) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii ya Zanzibar (Zati), Jumuiya ya Waendeshaji Watalii Zanzibar (Zato) na Jumuiya ya wenye hoteli ya Zanzibar (HAZ).

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha