99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa kibinadamu kwa Somalia

(CRI Online) Januari 31, 2024

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema Umoja huo umezindua mpango wa mwaka 2024 wa mahitaji na mwitikio wa kibinadamu nchini Somalia, unaohitaji dola bilioni 1.6 za Kimarekani ili kusaidia watu milioni 5.2 nchini humo.

Msemaji huyo amesema mwaka jana Somalia ilikumbwa na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ukame mkali, mvua na mafuriko makubwa ambavyo havijawahi kukutokea kabla, na kusababisha watu kukimbia makazi yao. Mbali na hayo, mamilioni ya watu waliendelea kukabiliwa na njaa na utapiamlo.

Amesema Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imeonya kuwa watu zaidi ya milioni 4, ambao ni karibu robo ya watu wanaoishi nchini humo, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha