

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje ya China asema China na Thailand kuingia "zama ya kusameheana?visa,"
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akisaini makubaliano ya kusameheana visa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand, Parnpree Bahiddha-Nukara baada ya mashauriano ya kila mwaka mjini Bangkok, Thailand, Januari 28, 2024. (Xinhua/Wang Teng)
BANGKOK - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema siku ya Jumapili katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya kila mwaka na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Parnpree Bahiddha-Nukara kwamba China na Thailand zitaingia rasmi katika "zama ya kusameheana visa" kuanzia Machi 1 kwani pande hizo mbili zimetia saini makubaliano ya kusameheana visa huku akisema uamuzi huo bila shaka utaleta mawasiliano baina ya watu ya pande mbili kwenye kilele kipya.
“Kutakuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watalii wa China wanaotembelea Thailand. Pia tunakaribisha watu kutoka Thailand ili kuhisi ustawi na uzuri wa China na ukarimu wa watu wa China. China na Thailand ni familia moja. Ni muhimu kwamba watu wetu wa pande mbili wajenge urafiki wa karibu na uhusiano wenye nguvu zaidi, na kukumbatia maisha bora,” Wang amesema.
Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema pande hizo mbili zimebadilishana maoni kwa kina kuhusu utekelezaji wa matokeo ya mikutano kati ya viongozi wa China na Thailand na ujenzi wa Jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja, na kufikia makubaliano.
Wang amesema kuwa China siku zote inaichukulia Thailand kama kipaumbele katika diplomasia yake na nchi jirani.
Amesema China inapongeza Thailand kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuunga mkono kikamilifu Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.
Wang amesisitiza kuwa, kwa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Thailand, uhusiano huo utafikia hatua mpya ya mwanzo wa kihistoria.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma