99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mwanadiplomasia Mkuu wa China Wang Yi akutana na mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 29, 2024

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akifanya mazungumzo na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan mjini Bangkok, Thailand, Januari 26, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

BANGKOK - Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amefanya duru mpya ya mazungumzo na Mshauri wa Mambo ya Usalama wa Marekani Jake Sullivan siku ya Ijumaa na Jumamosi mjini Bangkok, Thailand ambapo pande hizo mbili zilikuwa na mawasiliano ya kimkakati ambayo ni ya dhati, muhimu na yenye manufaa kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili huko San Francisco na kushughulikia ipasavyo masuala muhimu na ya nyeti katika uhusiano kati ya China na Marekani.

Wang, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC amebainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani, na kwamba pande zote mbili zinapaswa kuchukua fursa hii kupata uzoefu na somo, kutendeana kwa usawa badala ya kudharauliana.

Wang amesisitiza kuwa suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya China, na uchaguzi wa hivi karibuni katika eneo la Taiwan hauwezi kubadilisha ukweli wa kimsingi kwamba Taiwan ni sehemu ya China.

Hatari kubwa zaidi kwa amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan inatokana na "kujitenga kwa Taiwan", ambayo pia inaleta changamoto kubwa kwa uhusiano kati ya China na Marekani. Amesema, upande wa Marekani lazima ufuate kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa rasmi tatu za pamoja kati ya China na Marekani, kuweka dhamira yake kwa vitendo ya kutounga mkono "kujitenga kwa Taiwan" na kuunga mkono kuungana tena kwa amani kwa China.

Kwenye mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimekubaliana kutekeleza kwa pamoja maono ya San Francisco: viongozi wa nchi hizo mbili watadumisha mawasiliano ya mara kwa mara ili kutoa mwongozo wa kimkakati kwa uhusiano wa pande mbili; kuhimiza mabadilishano katika nyanja mbalimbali na katika ngazi mbalimbali kati ya China na Marekani.

Pande hizo mbili pia zimejadili masuala ya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mashariki ya Kati, Ukraine, Peninsula ya Korea na Bahari ya Kusini ya China.

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akifanya mazungumzo na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan mjini Bangkok, Thailand, Januari 26, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, akifanya mazungumzo na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan mjini Bangkok, Thailand, Januari 26, 2024. (Xinhua/Wang Teng)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha