99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yapongeza juhudi za Harakati ya Muungano wa?Nchi Zisizofungamana na Upande wowote katika kuendeleza amani duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2024

KAMPALA - Mwakilishi Maalum wa Rais Xi Jinping wa China Liu Guozhong amehudhuria Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi za Harakati ya Muungano wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) Ijumaa na Jumamosi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, ambapo ametoa hotuba akiangazia jukumu muhimu la harakati hiyo katika kuhimiza lengo kuu la amani ya Dunia na maendeleo ya binadamu.

NAM, iliyoanzishwa katika kilele cha harakati za ukombozi wa kitaifa katika mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya Kusini, imeendeleza ipasavyo mambo ya amani ya Dunia na maendeleo ya binadamu, amesema Liu, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Naibu Waziri Mkuu wa Baraza la Serikali la China.

Inapaswa kuendelea kushikilia uhuru na kupinga siasa za kugombea madaraka, kutafuta maoini ya pamoja huku ikiondoa tofauti, kuhimiza kuishi kwa pamoja kwa amani, kujiendeleza kupitia mshikamano, kujitahidi kutafuta maendeleo ya pamoja, na kutetea usawa na haki, Liu amesema.

Liu amesisitiza kuwa China daima itakuwa moja ya nchi zinazoendelea na inapenda kushirikiana na nchi wanachama wa NAM kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia chini ya mwongozo wa kujenga jumuiya ya kimataifa yenye mustakabali wa pamoja.

Amesema China itaendeleza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kutekeleza maadili ya pamoja ya binadamu, na kutetea Dunia yenye ncha nyingi yenye usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote, ili kuiendeleza Dunia kuelekea mustakabali mzuri wa amani, usalama, ustawi na maendeleo.

Wakuu wa nchi na serikali na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka nchi zaidi ya 100, na wakuu wa mashirika ya kimataifa walihudhuria mkutano huo. Siku ya Jumamosi, Liu alialikwa kuhudhuria semina ya Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuhusu maendeleo iliyoandaliwa na Rais Museveni na kutoa hotuba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha