99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mkurugenzi mkuu wa IMF asema ongezeko la pato la taifa la China ni “habari nzuri” kwa dunia

(CRI Online) Januari 19, 2024

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Bibi Kristalina Georgieva alipohojiwa kando ya mkutano wa 54 wa kila mwaka wa Baraza la Uchumi Duniani huko Davos, amesema ongezeko la uchumi wa China katika mwaka 2023 ni habari nzuri kwa China na nchi nyingine.

Amesema uchumi wa China umefikia lengo lake la ongezeko la takriban asilimia 5, na kuvuka lengo hilo, hali ambayo ni habari nzuri kwa China, Asia na dunia nzima, kwani China imefikia mchango wa theluthi moja ya ongezeko la dunia.

Ameongeza kuwa serikali ya China inadhamiria ongezeko la uchumi lililo bora, kwa kubadilisha tegemeo la ongezeko la uchumi kutoka uuzaji nje wa bidhaa na kuwa matumizi katika manunuzi.

Idara ya takwimu ya China Jumatano ilitangaza kuwa pato la taifa la China kwa mwaka 2023 limeongezeka kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita, na thamani yake inafikia yuan trilioni 126.06 (sawa na dola takriban trilioni 17.71 za kimarekani).

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha