

Lugha Nyingine
Marekani yaorodhesha tena kundi la waasi la Houthi kuwa magaidi
Ikulu ya Marekani, White House ikionekana wakati wa kuanguka kwa theluji mjini Washington, D.C., Marekani, Januari 15, 2023. (Picha na Aaron Schwartz/Xinhua)
WASHINGTON - Marekani imeliorodhesha tena kundi la waasi wa Houthi kuwa kundi la kigaidi siku ya Jumatano, kwa mara nyingine tena ikiliita kile kinachoitwa Kundi Maalumu Lililoorodheshwa la Kigaidi Duniani (SDGT) ambapo Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani Jake Sullivan amesema katika taarifa kwamba uamuzi huo ni sehemu ya kujibu vitisho vya Wahouthi vinavyoendelea na mashambulizi dhidi ya "vikosi vya kijeshi vya Marekani na meli za kimataifa zinazofanya kazi katika Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden."
Sullivan amesema kitendo hiki "kitazuia ufadhili wa kigaidi kwa Wahouthi, kuzuia zaidi ufikiaji wao wa masoko ya kifedha, na kuwawajibisha kwa vitendo vyao." Ameongeza kuwa ikiwa Wahouthi watasitisha mashambulizi yao, "Marekani itatathimini mara moja uamuzi huo."
Uamuzi huo utaanza kutekelezwa katika siku 30 zijazo, Sullivan amesema. Muda kati ya sasa na wakati wa uamuzi huo kutakapoanza kutekelezwa utairuhusu Marekani "kuhakikisha njia za misaada ya kibinadamu zinapatikana ili hatua yetu ilenge Wahouthi na siyo watu wa Yemen," ameongeza.
Afisa huyo amesema alipozungumza na waandishi wa habari kwamba mashambulizi ya Houthi dhidi ya meli za kimataifa ni "mfano wazi wa ugaidi kukiuka sheria za kimataifa na ni tishio kubwa kwa maisha na biashara ya kimataifa," na kuongeza kuwa "yanahatarisha usafirishaji wa misaada ya kibinadamu."
Amesema “Lengo la mwisho" la hatua ya Marekani, ni "kuwashawishi Wahouthi kupunguza mashambulizi na kuleta mabadiliko chanya katika kitendo chake. Marekani inaweza kufikiria kuliondoa kutoka kwenye orodha hii wakati kundi la Houthi kusitisha mashambulizi yao”
Januari 10, 2021, serikali ya Marekani ilitangaza mojawapo ya sera zake za mwisho za kigeni kwa kuliorodhesha kundi la waasi la Houthi kwenye orodha ya makundi ya kigaidi.
Mwezi Februari 2021, serikali ya rais wa sasa Joe Biden ulibatilisha uamuzi huo, ukisema uamuzi huo ulikuwa ni "utambuzi wa hali mbaya ya kibinadamu nchini Yemen."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma