

Lugha Nyingine
China yapinga vikali Marekani kupitisha sheria kuhusu suala la Taiwan
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bi. Mao Ning amesema China inapinga vikali Marekani kupitisha kile inachoita sheria inayohusiana na Taiwan, na imetoa malalamiko makali kwa upande wa Marekani.
Kwa mujibu wa habari zilizoripotiwa, Baraza la Wawakilishi la Marekani hivi majuzi lilipitisha Sheria ya Kutobagua ya Taiwan ya 2023, inayomtaka Waziri wa Fedha wa Marekani kutumia ushawishi wa Marekani katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kuunga mkono uanachama wa Taiwan katika shirika hilo.
Akijibu swali linalohusiana na suala hilo, Bi. Mao amesema Marekani kupitisha sheria hiyo ni kitendo cha kuingilia mambo ya ndani ya China na kujaribu kutumia suala la Taiwan kwa madhumuni ya kisiasa kwa lengo la kuwa na "China mbili" yaani "China moja, Taiwan moja". China inapinga vikali na imetoa malalamiko makali kwa upande wa Marekani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma