99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri Mkuu wa China asema China itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya

(CRI Online) Januari 17, 2024

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema China iko tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), na kushughulikia ipasavyo tofauti zilizopo kati ya pande mbili chini ya kanuni ya kuelewana na kuheshimiana.

Bw. Li amesema kwenye dunia ya leo ambayo imejaa mabadiliko na misukosuko, uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya bado upo thabiti katika uhusiano kati ya nchi kubwa, jambo ambalo linatokana na juhudi za pamoja. Bw. Li amesema alipokutana na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen kando ya Mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia 2024.

Bw. Li amesema Rais wa China Xi Jinping alivyosema, uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya una umuhimu wa kimkakati na ushawishi wa kimataifa, na kuongeza kuwa kuimarisha uhusiano kati ya China na EU daima ni kipaumbele cha kidiplomasia kwa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha