99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Marekani na Uingereza zafanya mashambulizi mapya dhidi ya Hodeidah nchini Yemen

(CRI Online) Januari 15, 2024

Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi mapya dhidi ya mji wa bandari ya Hodeidah katika Bahari Nyekundu nchini Yemen, wakati ndege za kivita za nchi hizo zikiendelea na mashambulizi katika Mlima Jad'a, wilaya ya Alluheyah kaskazini mwa mji huo.

Mashambulizi hayo ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani na Uingereza katika siku tatu zilizopita.

Marekani na Uingereza zimeeleza kuwa mashambulizi hayo ni hatua za kulizuia kundi la Houthi la Yemen kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya meli za kimataifa katika Bahari Nyekundu, ambayo ni njia muhimu ya biashara ya kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha