99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Faharisi ya kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kwenye pwani za China yaongezeka Mwezi Desemba, 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024

Picha hii iliyopigwa Desemba 27, 2023 ikionyesha gati la kiotomatiki la Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Picha na Zhang Jingang/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Desemba 27, 2023 ikionyesha gati la kiotomatiki la Bandari ya Qingdao, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China. (Picha na Zhang Jingang/Xinhua)

SHANGHAI--Faharisi ya kiwango cha usafirishaji wa bidhaa kwenye pwani za China ilipanda kwa asilimia 11.9 Mwezi Desemba 2023 kuliko mwezi uliotangulia, takwimu kutoka Idara ya Biashara ya Usafirishaji ya Shanghai (SSE) zimeonyesha, na mwezi wa Desemba faharisi jumuishi ya kiwango hicho katika maeneo ya pwani, ambayo hupima gharama za usafirishaji katika soko la usafirishaji wa meli wa pwani, ilikuwa 1,135.21.

Katika kipindi hicho, faharisi ndogo kwa usafirishaji wa makaa ya mawe ilipata ongezeko kubwa zaidi la asilimia 15.8 kuliko kipindi kama hiki cha mwaka uliopita, ikifuatiwa na ile ya nafaka na madini ya chuma.

Faharisi ndogo ya mafuta ghafi iliongezeka kwa asilimia 0.5 kuliko mwezi uliopita, wakati ile ya mafuta yaliyosafishwa iliongezeka kwa asilimia 2 kwa mwezi.

SSE ilianzisha utoaji wa faharisi hiyo Mwaka 2001 chini ya uongozi wa Wizara ya Usafirishaji na Uchukuzi ya China ili kuakisi kikamilifu mabadiliko ya soko la usafirishaji wa pwani la China.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha