99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

ADB yaongeza makadirio ya ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2023 hadi asilimia 5.2

(CRI Online) Desemba 14, 2023

Ripoti ya "Makadirio ya Maendeleo ya Asia 2023 (Toleo la Desemba)" iliyotolewa Jumanne wiki hii na Benki ya Maendeleo ya Asia imekadiria kuwa kiwango cha ukuaji wa uchumi wa China cha mwaka huu kitafikia asilimia 5.2, ikiwa ni zaidi ya makadirio ya awali ya ukuaji wa asilimia 4.9 yaliyotolewa mwezi Septemba.

Ripoti hiyo imesema uchumi wa China umedumisha kasi ya ukuaji katika robo ya tatu ya mwaka, ukichochewa na mambo kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa matumizi ya kaya na uwekezaji wa umma.

Ripoti hiyo pia imekadiria kuwa, uchumi wa nchi zinazoendelea katika eneo la Asia-Pasifiki utakua kwa asilimia 4.9 mwaka huu, ikiwa ni asilimia 0.2 zaidi ya makadirio ya mwezi Septemba, na utakua kwa asilimia 4.8 mwaka 2024, sawa na makadirio ya awali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha