

Lugha Nyingine
Mkuu wa UN kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi atoa wito wa kuunganisha juhudi kufikia "matokeo" ya mwisho ya mkutano wa COP28
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi Simon Stiell akizungumza na wanahabari kwenye Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 11, 2023. (Christopher Pike /COP28/ Xinhua)
DUBAI - Wakati mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa COP28 ukiingia katika hatua yake ya mwisho, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi Simon Stiell Jumatatu ametoa wito kwa pande zote kuunganisha juhudi kuelekea "matokeo" ya mwisho ya mkutano huo.
"Hatuna dakika ya kupoteza katika kipindi hiki muhimu cha mwisho," Stiell amewaambia waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa bado kuna nafasi kwa watu wanaojadili "kuanzisha ukursa mpya -- ambao unaleta manufaa kwa watu na sayari."
Amesema mijadala inaendelea juu ya masuala mawili muhimu: matarajio ya nchi juu ya kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na nia yao ya kuunga mkono kubadilisha muundo wa nishati kwa njia sahihi ya uungaji mkono.
Huku akieleza kuwa "Ninashinda, umeshindwa ' ni kichocheo cha kushindwa kwa pamoja," ametoa wito wa kuondoa ufungaji wa kimbinu usio wa lazima , kukataa utetezi wa kufanya mageuzi hatua kwa hatua, na kulinda na kuheshimu viti vya kila upande kwenye majadiliano, kanuni muhimu ni ujumuishaji, uwakilishi, na uwazi, pamoja na kuwasilisha matokeo bora zaidi mbele na kati.
Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unatarajiwa kuhitimishwa leo Jumanne, huku mswada mpya wa makubaliano tarajiwa ya mwisho ukitolewa.
Hata hivyo, makubaliano hayo ya mwisho yanaweza tu kupitishwa kutokana na makubaliano kati ya nchi karibu 200 zilizopo.?
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi Simon Stiell akizungumza na wanahabari kwenye Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Desemba 11, 2023. (Christopher Pike/COP28/ Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma