99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China kufanya kila juhudi kulinda raia, kutuliza mgogoro, na kuanzisha tena mazungumzo ya amani huko Gaza

(CRI Online) Novemba 09, 2023

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema siku ya Jumatano kuwa China ikiwa ni mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na nchi mwanachama inayowajibika katika jumuiya ya kimataifa, itaendelea kufanya mawasiliano na pande husika katika mgogoro wa Israel na Palestina na kufanya juhudi zote kulinda raia, kutuliza mgogoro, kuanzisha upya mazungumzo ya amani, na kutimiza amani.

Bw. Wang Wenbin amesema China inaomboleza vifo vya watu wa Palestina na Israel waliopoteza maisha katika mgogoro huo, na kusema matumizi ya nguvu hayawezi kuleta usalama na amani ya kudumu.

Amesema, kuwaachilia mateka, kulinda usalama wa raia na vifaa vya kiraia, kufungua njia za misaada ya kibinadamu, na kuanzisha tena mazungumzo ni jukumu la pande husika na pia ni dhamira ambayo jumuiya ya kimataifa inapaswa kujitahidi kuifikia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha