99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uganda na China zasaini makubaliano ya kuendeleza matumizi ya intaneti nchini Uganda

(CRI Online) Novemba 01, 2023

Uganda na China zimesaini makubaliano ya kuharakaisha maendeleo, ushirikiano na mageuzi ya kidijitali nchini Uganda ambayo yamesainiwa mjini Beijing, ambako kongamano la ushirikiano wa kujenga uwezo wa kidijitali kati ya China na Afrika linafanyika.

Waziri wa Habari, Teknolojia ya Mawasiliano na Mwongozo wa Kitaifa wa Uganda Dkt. Chris Baryomunsi, amesema serikali ya Uganda imekuwa ikishirikiana na China kuweka uti wa mgongo wa miundombinu ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya intaneti. Amesema China imepiga hatua kwenye teknolojia na imekuwa muhimu katika kusambaza kebo za intaneti nchini Uganda.

Amesema kupitia ushirikiano huu, wataweza kujenga miundombinu mipya, vifaa, mafunzo na kutoa huduma kwa waganda wote.

Dk. Baryomunsi amesema kwa sasa wanaunganisha maeneo ya mijini na vijijini kwa kutumia kampuni za China na kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma huku serikali ikitaka kila mtu afurahie huduma ya intaneti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha