99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Kampuni 30 za China kushiriki katika Wiki ya Mitindo ya Mavazi ya Afrika

(CRI Online) Novemba 01, 2023

Kampuni 30 za China zinatarajiwa kushiriki katika Wiki ya 9 ya Maonyesho ya Ubunifu wa Mavazi ya Afrika (ASFW), ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 3 hadi 6 mwezi huu mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Shirikisho la Watengenezaji wa Vitambaa na Nguo la Ethiopia, Goshu Negash amesema, maonyesho hayo ya kimataifa ya siku nne yatakutanisha waagizaji zaidi ya 300 wanaojihusisha na sekta za nguo, ngozi, teknolojia na mapambo ya ndani, na kwamba kati yao, washiriki 30 wanatoka nchini China.

Amesema maonyesho hayo ya mwaka huu yatahusika na ajenda muhimu za sekta hiyo, ikiwemo Eneo la Biashara Huria la Afrika, uzalishaji endelevu na nafasi ya teknolojia za akili bandia katika maendeleo ya viwanda vya nguo na vitambaa barani Afrika.

Amesema watengenezaji wa vitambaa kutoka China wanachukua nafasi muhimu katika maendeleo ya sekta ya nguo na vitambaa ya Ethiopia, wakitoa nafasi za ajira na kuhamisha teknolojia kupitia maeneo yao maalum ya viwanda yaliyoko Dukem, Adama na Dire Dawa nchini Ethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha