

Lugha Nyingine
Benki Kuu ya Tanzania yasema ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo uko katika mwelekeo sahihi
(CRI Online) Novemba 01, 2023
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuwa, ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo uko katika mwelekeo sahihi kufikia ukuaji wa asilimia 5.3 katika mwaka 2023.
Katika taarifa yake iliyotolewa Jumanne, Benki hiyo imesema ukuaji wa uchumi katika robo ya kwanza na ya pili ya mwaka huu umekuwa wa kuridhisha, ukifikia asilimia 5.4 na 5.2.
Taarifa hiyo pia imesema, uchumi wa visiwani Zanzibar umekua kwa asilimia 6.2 katika robo ya kwanza ya mwaka 2023, na unatarajiwa kufikia lengo la ukuaji la mwaka la asilimia 7.1.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma