99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rais wa China asema binadamu ni jamii yenye mustakabali wa pamoja

(CRI Online) Oktoba 18, 2023

(Picha inatoka Xinhua.)

(Picha inatoka Xinhua.)

Rais wa China Xi Jinping amesema, binadamu ni jamii yenye mustakabali wa pamoja.

Akizungumza leo hapa Beijing, rais Xi amesema China inaweza kufanikiwa pale dunia nzima inapofanikiwa, na kwamba China inapofanya vizuri, dunia itakuwa nzuri Zaidi.

Rais Xi amesema, kupitia ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, China inafungua mlango wake zaidi kwa dunia, huku mikoa yake ikibadilika kutoka kuwa ya nyuma hadi kusonga mbele, na maeneo ya pwani yakipanda ngazi mpya katika ufunguaji wa mlango.

Amesema China imekuwa mwenzi muhimu wa biashara kwa zaidi ya nchi na sehemu 140 duniani, na ni moja ya chanzo kikuu cha uwekezaji kwa nchi nyingi zaidi. Ameongeza kuwa, uwekezaji wa China kwa nchi za nje na uwekezaji wa kigeni nchini China vyote vimeboresha urafiki, ushirikiano, hali ya kuaminiana na matumaini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha