99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema China na Iran zitasaidiana katika maslahi ya msingi

(CRI Online) Agosti 21, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi amesema China iko tayari kuendelea kushirikiana na Iran ili kusaidiana kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi.

Akiongea kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian siku ya Jumapili, Bw Wang ameongeza kusema kuwa wakati Rais Ebrahim Raisi wa Iran alipofanya ziara ya kiserikali nchini China Mwezi Februari mwaka huu, wakuu wa nchi hizo mbili walifikia makubaliano mapya muhimu kuhusu ushirikiano wa pande mbili, jambo ambalo lilipelekea uhusiano wa China na Iran kufikia ngazi mpya.

Aidha Bw. Wang amesema China pia iko tayari kuendelea kushirikiana na Iran kupinga kwa pamoja uingiliaji kati wa nje, kupinga ukandamizaji unaofanywa na upande mmoja, kutetea mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi hizo mbili na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na haki ya kimataifa.

Naye Amir-Abdollahian amesema, Iran inatilia maanani sana maendeleo ya ushirika wa kimkakati wa pande zote kati ya Iran na China, na inatazamia kudumisha mawasiliano ya hali ya juu na China, kuzidisha ushirikiano chini ya ‘Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja’ na kuimarisha uratibu na ushirikiano katika masuala ya kimataifa na kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha