99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Rwanda yaadhimisha siku ya mavuno kwa kuimarisha umoja na kuondoa umasikini katika familia

(CRI Online) Agosti 07, 2023

Rwanda imesherehekea Siku ya Kitaifa ya Mavuno, kwa lengo la kuwashawishi Wanyarwanda kufanya juhudi ili kuimarisha umoja wa kitaifa, kuondoa umasikini katika familia, na kutimiza ustawi.

Siku hiyo ambayo huadhimishwa Ijumaa ya kwanza ya mwezi Agosti kila mwaka, ni ya kitamaduni na ina lengo la kusherehekea mavuno.

Akizungumza katika sherehe hiyo, Waziri wa Kilimo na Rasilimali ya Mifugo nchini humo Idelphonce Musafiri, amesema lengo la kuadhimisha siku hiyo ni kwa ajili ya Wanyarwanda kukusanyika pamoja, kuwasiliana, na kupongezana kwa mafanikio makubwa waliyopata. Pia kuwatia moyo kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha waweze kudumisha na kujenga mafanikio yao kwa ajili ya siku za baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha