99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Watu 12 wafariki baada ya jengo kuanguka nchini Cameroon

(CRI Online) Julai 24, 2023

Watu 12 wamefariki na wengine 19 kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nne kuanguka kwenye eneo la kibiashara la Douala, nchini Cameroon, mapema jana.

Gavana wa Jimbo la Littoral Ivaha Diboua amesema, kati ya watu waliofariki ni wanawake na watoto, na kuongeza kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kuwatafuta watu waliokwama kwenye kifusi.

Amesema jeshi, kikosi cha zimamoto, polisi na vikosi vyote vya usalama vinashirikishwa katika kazi ya uokoaji, na kwamba huenda idadi ya watu waliofariki ikaongezeka.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha