99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Asilimia 26 ya idadi ya watu nchini Botswana wanakabiliwa na ukosefu wa usalama

(CRI Online) Julai 20, 2023

Idadi ya watu nchini Botswana wanaokabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula imeongezeka na kufikia asilimia 26.16 mwaka 2022 kutoka asilimia 20.16 iliyorekodiwa mwaka 2021.

Takwimu zilizotolewa jana na Idara ya Takwimu ya nchini humo zimeonyesha kuwa, idadi ya watu wanaokabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula kwa mwaka 2019 ilikuwa ni asilimia 22.20.

Mtaalamu wa kilimo nchini Botswana Brian Motshoganetsi ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa, mchanganyiko wa athari za mabadiliko ya tabianchi na janga la COVID-19 vimeongeza ukosefu wa usalama wa chakula nchini humo, na kuongeza kuwa, Botswana inapaswa kuwa na mawazo ya kimkakati yanayolenga kuongeza uzalishaji wa chakula ndani ya nchi hiyo kuliko kutegemea kuagiza kutoka nje.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha